Trump, Starmer wasaini mikataba mikubwa ya uwekezaji
18 Septemba 2025
Matangazo
Viongozi hao wawili wamesaini mkataba mkubwa wa uwekezaji katika teknolojia, ikiwemo akili bandia na nishati ya nyuklia, mkataba ambao unatarajiwa kuleta maelfu ya ajira na mabilioni ya fedha za uwekezaji.
Hapo jana, Trump na mkewe Melania walipokelewa kwa heshima kubwa na Mfalme Charles wa Tatu na Malkia Camilla katika kasri la Windsor, ikiwa ni mara ya kwanza kwa rais wa Marekani au kiongozi yeyote wa dunia kualikwa kwa mara ya pili katika ziara ya kiserikali.
Waziri Mkuu Starmer alisisitiza urafiki na heshima ya kweli kati yake na Trump, akisema ni heshima kumkaribisha kiongozi huyo wa Marekani aliyemuita rafiki yake.