1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

FBI: "Trump amelengwa kwenye jaribio la kuuawa."

16 Septemba 2024

Mgombea wa urais nchini Marekani kupitia chama cha Republican Donald Trump yuko salama baada ya risasi kadhaa kufyatuliwa karibu na uwanja alikokuwa akicheza mpira wa gofu huko West Palm Beach, Florida jana Jumapili.

Uchaguzi Marekani | Trump akiwa Tucson
Mgombea wa urais nchini Marekani Donald Trump amejikuta tena kwenye kile kinachotajwa kama jaribio la kumuua, septemba 16, 2024 Picha: Alex Brandon/AP Photo/picture alliance

Shirika la Upelelezi nchini humo, FBI, limesema Trump, alilengwa katika kile walichokitaja kama "jaribio la kumuua."

Idara ya Usalama wa Taifa na FBI wamesema wanachunguza tukio hilo lililotokea muda mfupi kabla ya saa nane za mchana, kwa majira ya eneo hilo.

Rais Joe Biden amekemea kitendo hicho akisema siasa za Marekani hazina nafasi ya machafuko na kuiagiza Idara ya Usalama wa Taifa kutumia kila rasilimali kumlinda Trump.

Trump alijeruhiwa kwa risasi sikioni, katika jaribio la kumuua la Julai 13 huko Pennysylvania, na kuibua maswali kuhusiana na usalama wa wagombea urais, miezi kidhaa kabla ya kufanyika uchaguzi.