1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi aahidi mageuzi DRC

Salehe Mwanamilongo13 Desemba 2019

Rais Tshisekedi ameahidi mageuzi hayo ya kisheria na katiba kuhusu kuwepo na duru mbili za uchaguzi wa urais na vilevile uwezekano wa kuwa na uraia wa nchi mbi

Präsident des Kongos: Felix Tshisekedi
Picha: Getty Images/AFP/S. Maina

Akilihutubia taifa kwa mara kupitia bunge pamoja na seneti tangu alipoapishwa kuwa rais wa Kongo mapema mwaka huu, Tshisekedi ameomba pia kuongezwa nguvu kwa kikosi maalumu cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO, kwa ajili kuwalinda raia wa Kivu ya Kaskazini.

Kwenye hotuba wake rais Felix Tshisekedi amesema kwamba kuna umuhimu wa kueko na mageuzi ya katiba ambayo yatawezesha kueko na duru mbili ya uchaguzi wa rais. Katiba ya hivi sasa ina duru moja pekee ya uchaguzi wa rais na mgombea anaweza kuchaguliwa kuwa rais angalau na asimilia 15 za kura.

Mageuzi mengine anayoahidi ni yale ya kuwepo na uraia wa nchi mbili. Swali hilo lilizusha tofauti kubwa mwaka wa 2003 ambapo katiba ailielezea kwamba raia wa Kongo hawezi kuwa na uraia wa nchi mbili.

Kuhusu usalama wa nchini rais Tshisekedi amesifu hatua iliofikiwa katika kuyasaka makundi ya wapiganaji huko Kivu ya kasazini na Kivu ya kusini, lakini amesema kwamba bado yapo mengi yakufanywa. Rais Tshisekedi amelaani kuvamiwa kwa kikosi cha kulinda amani cha umoja wa mataifa MONUSCO kufuatia maaanadamano ya raia huko Beni huku akiomba kuwepo na ratiba ya kuondolewa kwa wanajeshi hao. Hata hivyo Tshisekedi amesema kwamba kikosi maalumu cha wanajeshi wa Monusco kutoka Afrika ya kusini, Malawi na Tanzania kupewa nguvu zaidi kwa ajili ya kuwakinga raia.

Mbali na hayo Felix Tshisekedi amelezea changa moto kubwa inayokabili Kongo, ambayo ni maendeleo yake ya kudumu. Amehaidi kupambana na rushwa ambayo amesema imekithiri katika sekta yote ya umma. Mwanzoni mwa hotuba wake wa masaa mawili na nusu rais Tshisekedi alisifu kile alichoita kuwa ni ujasiri wa mtangulizi wake Joseph kabila amabae alaiachia madaraka kulingana na katiba. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW