1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi aishutumu Rwanda kwa kukiuka mkataba wa amani

8 Desemba 2025

Rais wa Kongo Felix Tshisekedi ameishutumu Rwanda kwa kukiuka wajibu wake chini ya makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Marekani.

Picha ya Pamoja | Paul Kagame na Felix-Antoine Tshisekedi Tshilombo
Picha ya pamoja ya Rais Paul Kagame wa Rwanda na Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: Virginia Mayo/AP/picture alliance

Tshisekedi amesema hayo alipowahutubia wabunge hii leo Jumatatu na kuongeza kuwa hatua hiyo inadhoofisha juhudi za kumaliza mapigano mashariki mwa Kongo.

Marais wawili Tshisekedi na Paul Kagame wa Rwanda walisaini makubaliano ya amani mjini Washington wiki iliyopita, mbele ya Rais wa Marekani Donald Trump unaolenga kuumaliza mzozo uliodumu kwa zaidi ya miongo mitatu katika eneo hilo lenye utajiri wa madini.

Hata hivyo kumeripotiwa mapigano makali kwenye eneo hilo licha ya makubaliano hayo, na kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu, karibu raia 20 waliojeruhiwa waliondolewa kati ya Jumamosi na Jumapili kutoka kwenye eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW