1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi ajitangaza rasmi kuwa rais, ataka jeshi limuheshimu

Mohammed Khelef19 Desemba 2011

Kiongozi mkuu wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Etienne Tshiseekdi, amejitangaza rasmi kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais licha ya uamuzi wa Mahakama Kuu wa hapo Ijumaa dhidi yake.

Kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi (kulia).
Kiongozi wa upinzani, Etienne Tshisekedi (kulia).Picha: picture-alliance/dpa

Tshisekedi amewaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa, kwamba serikali ya Rais Joseph Kabila imefutwa kazi na kwamba yeye, Tshisekedi, ndiye atakayeapishwa siku ya Ijumaa. Tshisekedi amewashukuru raia kwa kumchagua na kulitaka jeshi la Kongo kumtii.

Hata hivyo, msemaji wa chama tawala, ameiita kauli hiyo ya Tshisekedi kuwa ni utani mzaha mkubwa na kumuonya dhidi ya kuasi taasisi halali za Jamhuri.

Ijumaa iliyopita, Mahakama Kuu mjini Kinshasa iliamua kuwa Kabila alishinda uchaguzi kwa asilimia 49 ya kura dhidi ya asilimia 32 za Tshisekedi. Waangalizi wa kimataifa wanasema, uchaguzi wa Novemba 28 ulikuwa na dosari kubwa wakitaja matatizo yaliyojitokeza katika kuhisabu kura, na idadi kubwa ya kura ambazo hazikuonekana.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW