1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshisekedi akataa mazungumzo ya moja kwa moja na M23

19 Januari 2025

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi ameondowa uwezekano wa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na kundi la M23, akisema kwamba hatua hiyo italipa uhalali kundi hilo.

DR Congo | Félix Tshisekedi katika mahojiano na DW
Rais wa DRC Félix Tshisekedi akataa mazungumzo ya moja kwa moja na M23.Picha: DW

Kauli hii inajiri baada ya mkutano uliotarajiwa  kufanyika tarehe 15 Disemba nchini Angola kati ya Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame kufutwa wakati pande hizo mbili hazikuweza kukubaliana kuhusu masharti ya mazungumzo hayo.

Tshisekedi aliwaambia wanadiplomasia mjini Kinshasa kwamba mazungumzo hayo yameshindwa kwa sababu ya  ujumbe wa Rwanda kutowa sharti jipa la kutaka  yafanyike mazungumzo ya moja kwa moja kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kundi la waasi la M23.

Soma pia: UN: Zaidi ya watu 230,000 wamekimbia ghasia mashariki mwa DRC tangu Januari 1

Siku ya Alhamisi, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Angola Joao Lourenco walitoa wito wa kuanzishwa tena kwa mazungumzo katika ngazi ya juu kati ya DRC na Rwanda. Lakini Tshisekedi alisema nchi yake haitakubali kile alichokitaja kama "shinikizo kutoka nje" kuweka masharti ambayo yanakiuka kanuni na mamlaka ya Kongo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW