1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tshiseked aahidi uchaguzi wa kuaminika Kongo

18 Desemba 2023

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amesema uchaguzi mkuu wa siku ya Jumatano utafanyika katika mazingira ya kuaminika.

DRC| Rais Felix Tshisekedi
Rais Felix Tshisekedi amesema uchaguzi utafanyika katika mazingira ya kuaminika.Picha: Pool Vlad Vanderkelen/Belga/picture alliance

Lakini mivutano imeongezeka kutokana na ukosefu mkubwa wa maandalizi jambo linaloweza kusababisha migogoro katika taifa hilo. 

Kampeni zinakamilika rasmi leo wakati shirika la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch likitahadharisha kuwa ghasia zinazohusiana na zoezi hilo la upigaji kura zinatishia kuvuruga uchaguzi huo.

Soma pia: Kampeni za uchaguzi nchini Kongo kukamilika Jumatatu

HRW imesema vurugu hizo tayari zimesababisha kifo cha mtu mmoja.

Takriban watu milioni 44 ikiwa ni karibu nusu ya idadi jumla ya watu nchini humo, wanatarajiwa kumchagua rais ajaye wa Kongo katika uchaguzi wa nne tangu kumalizika mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na vya kikanda.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW