Tsunami yaua wengi Indonesia.
27 Oktoba 2010Matangazo
Kimbuka hicho cha tsunami iliyofikia urefu wa mita tatu, kimekuja dakika chache baada ya tetemeko la ardhi lililoikumba nchi hiyo siku ya Jumatatu.
Nyumba kadhaa zimeharibiwa kutokana na mawimbi hayo yaliyofika mita 600 katika nchi kavu.
Wakati huohuo watu 25 wamekufa baada ya mlima Merapi nchini Indonesia kulipuka mara tatu jana.
Hatua hiyo ilisababisha, maelfu ya watu kuyahama makaazi yao.