1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tsvangirai nchini Marekani.

12 Juni 2009

Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai anatafuta msaada wa kifedha ili kuufufua uchumi wa nchi yake.

Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai.Picha: AP

Waziri mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai leo anatarajiwa kukutana na Rais wa Marekani barack Obama mjini washington. Bw Tsvangirai huenda akaitumia nafasi hiyo anatarajiwa kuomba msaada wa fedha kwa nchi yake inayokabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi.Hata hivyo huenda Tsvangirai akajulishwa kuwa kunahitajika kufanyika mabadiliko zaidi nchini Zimbwe.

Mkutano wa leo unonyesha kibarua kigumu alichonacho rais Obama kuhusu kumsadia Tsvangirai kuujenga upya uchumi wa Zimbabwe uliozorota, bila ya kumpa msukumo wa kisiasa rais Robert Mugabe.

Nchi za magharibi zinamlaumu rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kwa kuiongoza vibaya Zimbabwe na kwa sehemu kubwa zimemtenga.

Obama aliiongezea vikwazo zaidi Zimbwbwe mwezi machi mwaka huu, akiwalenga washirika wa karibu wa rais Mugabe na baadhi makampuni ya ndani, lakini hata hivyo hajamtaka rais Mugabe kung`atuka madarakani kama ulivyokua ukitaka utawala wa mtangulizi wake rais Geroge Bush.

Tsvangirai ambaye hapo awali alikuwa afisa kwenye vyama vya wafanyakazi na kiongozi wa upinzani wa muda mrefu yuko nchini Marekani, kama moja wapo ya ziara zake barani ulaya kutafuta uungwaji mkono kwa serikali ya mseto aliyounda kati yake na rais Robert Mugabe mwezi Februari mwaka huu, baada ya kinyanganyiro kikali cha uchaguzi ambapo wafuaui wa Tsvangirai walipigwa na hata kufungwa.

Lakini Tsvangirai huenda huenda akarejea nyumbani mikono mitupu baada ya wafadhili kumfahamisha kuwa, wangependa kwanza kushuhudia mabadiliko nchini zimbabwe yakiwemo ya kiuchumi, kisiasa pamoja na ya kijamii.

Wazimbabwe wakinga`ng`ana kununua chakula.Picha: AP

Mataifa haya yanataka kuona madadiliko haya, ili kuhakikisha kuwa serikali ya mseto sio kifumba macho cha kuendeleza uongozi wa rais mugabe ambao sasa unakaribia kumaliza miongo mitatu, tangu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 85 aingie madarakani mwaka 1980.

Akihojiwa na shirika moja la habari la kimataifa, Tsvangirai alisema kuwa anaamini kuwa rais Obama atatoa ahadi ya misaada zaidi ya kibinadamu kwa mamilioni ya wazimbabwe wanaokabiliwa na ukosefu wa chakula, lakini akaongeza kuwa serikali mpya ya mseto haijafanya vya kutosha kulinda haki za binadamu na kuandaa uchaguzi ulio huru na wa haki.

Hatua muhimu zimepigwa nchini Zimbabwe tangu makubaliano ya kuundwa kwa serikali ya mseto yalipotiwa sahihi na chama cha waziri mkuu kujumuishwa serikalini. Lakini hata hivyo kuna mengi ambayo yanastahili kufanywa, alinukuliwa Mike Hummer, msemaji wa baraza la usalama wa taifa katika ikulu ya Marekani.

Ikulu ya marekani ilisema kuwa Tsvangirai na rais Obama wanatarajiwa kujadili mwelekeo mgumu unaoikabili Zimbabwe siku za usoni. Jana Alhamisi waziri wa Ujenzi nchini Zimbabwe alisema kuwanchi yake inahitaji zaidi ya dola bilioni mbili zitakazosaidia kubuni nafasi za ajira na kupunguza idadi ya wakosa ajira ambayo kwa sasa imefikia asilimia tisini.

Serikali ya Zimbabwe nayo inasema kuwa inahitaji dola bilioni kumi kuufufua uchumi wake ambao inasema kuwa utaimarika kwa asilimia mbili nukta nane mwaka huu.

Akiwahutubia watu walio na hekima wiki hii, Tsvangirai alisema kuwa mageuzi yaliyofanywa na serikali ya mseto yameleta mabadiliko yakiwemo ya kusitishwa kuchapishwa kwa dola ya Zimbabwe ili kuzuia kupanda kwa gharama ya maisha na kuwaondoa polisi wa kupambana na ghasia katika mitaa ya mji mkuu Harare.

Mwandishi :Jason Nyakundi

Mhariri :Mohammed Abdul Rahman