TULKAREM: Mahmoud Abbas aishutumu Israel
25 Agosti 2005Matangazo
Kiongozi wa wapalestina Mahmoud Abbas ameishutumu Israel kwa kuvuruga uwezekano wa kuwepo amani mashariki ya kati.
Matamshi ya bwana Abbas yanafuatia kuuwawa kwa wapiganaji watano wakipalestina na wanajeshi wa Israel katika kambi ya Tulakarem.
Mashambulio hayo ndio ya kwanza na mabaya zaidi kufanywa tangu kuanza kwa mpango wa Israel wa kuondoka Gaza.
Tukio hilo pamoja na mpango wa Israel wa kujenga kituo kikubwa kipya cha polisi kwenye eneo la magharibi mwa ukingo wa Gaza kumeondoa matumaini ya kimataifa kwamba kuondoka Gaza kwa Waisrael huenda kukasaidia kuufufua mpango wa amani wa mashariki ya kati.