Tume ya haki na maridhiano yaundwa Liberia
8 Januari 2008Kumeanzishwa tume ya haki na maridhiano nchini Liberia.
Nia ya tume hiyo ni kuchunguza madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2003.
Tume hiyo imeanza kazi huku kesi ya madai uhalifu wa kivita inayomkabili rais wa zamani wa nchi hiyo—Charles Taylor ikiwa imeingia siku yake ya pili mjini The Hague.
Tume ya Liberia, ya haki na maridhiano, inataka kufanana na ile ya Afrika Kusini ilioundwa baada ya kuondoa utawala wa ubaguzi wa rangi.
Hii itasikia kitu kama ushahidi kutoka watu 5000 wanaosemekana ni wahanga pamoja na watenda maovu. Hata hivyo raia wengi wa Liberia wanaipinga tume hiyo,wakisema itatonesha madonda ya wakati wa vita na ni baado mapema mno kuzindua kumbukumbu za wakati wa msukomsuko.
Lakini upande mwingine unaoiunga mkono,akiwemo rais Ellen Johnson Sirleaf,wanasema ni nguzo muhimu ya kupata amani ya kudumu nchini humo.
Kwa mujibu wa habari kutoka Liberia,watu saba wanaounda tume hiyo,mbali na kusikiliza kauli za wahusika,lakini hawatakuwa na uwezo wa kimahakama-wa kuwafungulia mashtaka wahusika.
Hata hivyo watafanya tu uchunguzi wa makosa yajinai pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vililipuka nchini Liberia mwaka wa 1989.Vilimalizika pale aliekuwa rais wakati huo,Samuel Doe kutimuliwa wapiganaji wa National Patriotic Front of liberia chini ya Bw Charles Taylor.
Ghasia zilizuka tena mwaka wa 1999 wakati waasi wakiungwa mkono na serikali jirani ya Guinea walipojitokeza kaskazini mwa Liberia kupinga utawala wa Taylor.Watu wapatao laki 2Unusu waliuliwa na wengine millioni 1 wakaachwa bila makazi katika mgogoro ulioendelea kwa kipindi cha miaka 14 mfululizo.
Taylor kwa sasa anakabiliwa na shtaka la uhalifu wa kivita mjini The Hague.
Mashataka ya uhalifu wa kivita dhidi ya Taylor sio kuihusu nchi yake ya Liberia bali nchi jirani ya Sierra Leone.
Anashtakiwa kwa kudhibiti na kuunga mkono kundi la wanamgambo ambalo mbali na ubakaji na ukataji waviungo vya raia maelefu kadhaa wa Sierra Leone lakini pia kuwauwa raia hao katika vita vya wewnyewe kwa wenyewe viliyotokea kuanzia mwaka wa 1991 hadi 2001.
Wanamgambo hao walitenda visa vyao wakifadhiliwa na almasi ambayo imekuja kujulikana kama almasi –damu kutokana na umwagikaji wa damu uliotokea wakati wa vita hivyo.
Shahidi wa kwanza,mtaalamu wa biashara ya almasi wakati wa migogoro Ian Smillie alitoa ushahidi wake.
Pia ilionyeshwa katika mahakama hiyo kulionyeshwa video ambapo wahanga walikatwa mikono na miuu na wapiganaji hao.
Lakini yeye wakili wa Bw Taylor Courtenay Griffins amepuuzia mbali ushahidi huo akisema upande wa mashtaka umeshindwa kulata ushihidi tosha sasa unatapatapa.
Taylor mwenyewe amekanusha madai hayo.Mwenyewe Taylor anahudhuria usikizwazi wa kesi yake ulipoanza rasmi jumatatu.
Na leo jumanne kesi hiyo imeingia siku ya pili mjini The Hague na pia hii ndio mara ya kwanza kwa kiongozi wa zamani wa Afrika kufika mbele ya mahakama ya kimatazifa kuhusu uhalifu wa kivita.