uamuzi wa kumruhusu Zuma kugombea wakatiwa rufaa
12 Aprili 2024Taarifa ya tume hiyo imesema imewasilisha rufaa hiyo mbele ya Mahakama ya Katiba ili chombo hicho kitoe uamuzi wa uhakika. Rufaa hiyo ni hatua nyingine kwenye mpambano wa kisheria juu ya uhalali wa Zuma kugombea uchaguzi wa Mei 29 kupitia chama kipya cha upinzani cha uMkhonto we Sizwe (MK).
Katika uamuzi wa kushangaza hapo siku ya Jumanne, mahakama inayoshughulikia mashauri ya uchaguzi iliamua kwamba Zuma mwenye umri wa miaka 81 anaweza kugombea, na kuufuata uamuzi uliotolewa kabla na tume ya uchaguzi wa kumpiga marufuku.
ANC yashindwa katika kesi dhidi ya chama cha Zuma
Tume hiyo ilimpiga Zuma marufuku kutokana na hatia aliyokutwa nayo ya kuipuuza mahakama na kuhukumiwa kwenda jela kwa miezi 15 mwaka 2021. Tume hiyo ilisema katiba ya Afrika Kusini inamzuia mtu yeyote aliyehukumiwa kifungo cha zaidi ya iezi 12 jela kuwania wadhifa wa kuchaguliwa.
Mawakili wake waliipinga hoja hiyo wakisema kifungo cha Zuma kilitokana na shauri lililoendeshwa kwa msingi wa kesi madai na siyo jinai.