1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tume ya uchaguzi Congo yatangaza ratiba ya uchaguzi mkuu

Jean Noel Ba-Mweze4 Februari 2022

Tume ya Uchaguzi nchini Kongo CENI imetangaza kuwa uchaguzi mkuu utafanyika ifikapo Desemba 2023. Hata hivyo,CENI ilisema kuwa ratiba hiyo haitaji tarehe rasmi za chaguzi hizo.

Kongo Beni improvisierte Wahlurne
Picha: Getty Images/AFP/A. Huguet

Awamu ya kwanza baina Januari 2022 na Desemba 2023 ni ule wa chaguzi za moja kwa moja za Rais wa Jamhuri, mabunge wa kitaifa na mikoa, washauri wa manispaa, pia viongozi wa sekta na wilaya.

Awamu ya pili baina Januari na Machi 2024 inajumuisha chaguzi zisizo za moja kwa moja za maseneta, magavana na makamu wao, washauri wa miji, mameya na makamu wao, viongozi wa manispaa na wale wa sekta. Na hatimaye, awamu wa tatu itakuwa muendelezo wa mchakato na hii kuanzia Machi 2024 hadi Machi 2027.

Soma pia:Kampeni za uchaguzi wa bunge zaanza Congo mashariki

Orodha ya masharti kabla ya uchaguzi

Ceni yataja masharti ya kifedha na kiusalama kwa kuandaa uchaguziPicha: Reuters/K. Katombe

Denis Kadima, mwenyikiti wa CENI alionyesha nia yake ya kuona uchaguzi wa rais na wabunge kufanyika kwa wakati, mnamo Desemba 2023, lakini hakutuliza mioyo kwani alitaja vikwazo kadhaa vikiwemo:

Vikwazo vya asili ya kisiasa na kiusalama, kutotambuliwa kwa uhuru wa kifedha wa CENI na kutokuwa na uhakika wa utoaji wa fedha na serikali, pia kuna uwezekano wa kutoheshimu ahadi za washirika wanaojiunga na ufadhili wa mchakato wa uchaguzi'', alisema Kadima.

Soma pia:

Mahakama yamtangaza Tshisekedi mshindi wa uchaguzi wa rais Congo

''Hawapendi kweli kwenda kwenye uchaguzi''

Congo bado kushuhudia chaguzi tulivuPicha: picture-alliance/AP Photo/J. Delay

Hata hivyo, upinzani unaipuuzilia ratiba hiyo na kukumbusha kuwa viongozi wa CENI waliwekwa bila makubaliano. Na kuhusu vikwazo vilivyotajwa, Augustin Mudekereza ambae ni Katibu Mkuu wa chama  MDVC, ameileza DW kwamba huo sasa ni ushahidi kwamba hakutakuwa na uchaguzi.

''Hakika kuna hiyo njama ambayo wanapanga ili uchaguzi usifanyike. Ukifuata hivyo vizuwizi ambavyo vinaweza kufanya uchaguzi usikuwe, sisi tunaona ya kwamba ni mambo walipanga, hawapendi kweli kwenda kwenyi uchaguzi.''

''Sisi kama chama cha upinzani tupo makini na tunawaambia waache kucheza na moto.'',alisema Mudekereza.

Aidha, CENI inapanga tarehe 6 Aprili ijayo, uchaguzi wa magavana na makamu wao hapa Kinshasa, Bas-Uélé, Haut-Lomami, Kasaï Oriental, Kongo Central, Lomami, Mai-Ndombe, Tanganyika, Maniema, Mongala, Tshopo, Kasai central na Kwango.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW