SiasaUganda
Tume ya uchaguzi: Rais Museveni anaongoza kwa asilimia 61.7
16 Januari 2026
Matangazo
Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa ndani ya saa 48 baada ya zoezi la upigaji kura kukamilika. Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Uganda baada uchaguzi mkuu wa rais na wabunge kufanyika hapo jana licha ya kasoro mbalimbali kushuhudiwa.
Lakini tayari mwanasiasa mkuu wa upinzani na anayegombea urais Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine anaishutumu serikali kwa "wizi wa kura" na kuwakamata baadhi ya maafisa wa chama chake. Baadhi ya kura zimeonekana kuhesabiwa kwa uwazi huku kukiwa hakuna vurugu zozote kubwa zilizoripotiwa.