1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaGeorgia

Tume ya uchaguzi yathibisha matokeo Georgia

16 Novemba 2024

Raia wa Georgia wameandamana Jumamosi baada ya tume ya uchaguzi kuthibitisha ushindi wa chama tawala katika kura ya bunge yenye utata iliyoambatana na madai ya uingiliaji wa Urusi na ulaghai.

Rais Salome Zurabishvili -Maandamano
Rais Salome Zurabishvili akosoa matokeo ya uchaguzi wa bunge.Picha: Alexander Patrin/TASS/IMAGO

Upinzani unaoungwa mkono na nchi za Magharibi umekosaoa kura hiyo ya Oktoba 26 na kusema ni ya "udanganyifu", huku Umoja wa Ulaya na Marekani zikitaka uchunguzi ufanyike kuhusu madai ya "ukiukwaji" katika uchaguzi.

Soma pia: Upinzani nchini Georgia waitisha maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi wa bunge

Matokeo ya mwisho yaliyotolewa leo Jumamosi ya tume ya uchaguzi yanakipa chama cha Georgian Dream ushindi wa viti 89 katika bunge lenye wabunge 150, ambalo upinzani unataja kuwa ni "haramu" na umekataa kuingia.

Rais Salome Zurabishvili -- akizozana na chama tawala -- pia ameitaja kura hiyo kuwa isiyo halali na kuishutumu Urusi kwa kuingilia kati. Moscow imekanusha madai hayo.

Kiongozi huyo mkuu alijiunga na miito ya upinzani ya kutaka kura mpya, akisema hatatoa amri ya kuitisha bunge jipya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW