Tunisia yafanya uchaguzi wa kwanza huru
23 Oktoba 2011Matangazo
Uchaguzi huo ambao ni wa kwanza huru katika historia ya Tunisia utaweka mfano kwa nchi nyengine za Kiarabu ambapo uasi umechochea mabadiliko ya kisiasa.Tunisia ndio ilioanzisha "Vuguvugu la Majira ya Machipuko ya Nchi za Kiarabu" miezi 10 iliopita wakati maandamano ya umma kupinga umaskini,ukosefu wa ajira na ukandamizaji wa serikali yalipomlazimisha Rais Ben Ali kukimbilia Saudi Arabia. Uchaguzi wa leo ni wa baraza la katiba ambalo litarasimu katiba mpya na pia kuteua serikali ya mpito na kupanga uchaguzi wa rais na bunge nchini humo.