1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaTunisia

Tunisia yatupilia mbali msaada wa kifedha wa Umoja wa Ulaya

3 Oktoba 2023

Rais wa Tunisia Kais Saied ameukataa hapo jana msaada wa kifedha wa dola milioni 133 uliotangazwa na Umoja wa Ulaya mwezi Septemba.

Tunesien Kais Saied
Picha: Tunisian Presidency/APA Images/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Rais Saied amesema kiasi hicho ni kidogo na kinakinzana na mkataba uliotiwa saini miezi mitatu iliyopita.

Mkataba wa mwezui Julai ulitoa ahadi ya msaada wa euro bilioni 1 kwa Tunisia ili kusaidia uchumi wake ulioathirika lakini pia kama sehemu ya mpango wa kupiga vita vitendo vya uhamiaji haramu.

Hivi karibuni maelfu ya wahamiaji waliwasili katika kisiwa cha Italia cha Lampedusa, wengi wao wakitokea fukwe za Tunisia.

Soma pia: EU kuilipa Tunisia chini ya mkataba wa kudhibiti uhamiaji

Hatua ya Saied inaweza kudhoofisha ushirikiano huo wa kimkakati, unaojumuisha hatua za kupambana na wasafirishaji haramu wa binaadamu na kuimarisha mipaka ya nchi hiyo ili kuzuia boti za wahamiaji wanaotaka kuingia barani Ulaya.