Janga
"Tupo pamoja nanyi" Klöckner, aliambia bunge la Ukraine
11 Machi 2026
Matangazo
Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kwanza katika taifa hilo linalokumbwa na vita.
Akiwa mwakilishi wa kwanza wa Ujerumani kulihutubia bunge la Ukraine, Klöckner aliwaambia wabunge kwamba Ujerumani siku zote ipo upande wao.
Julia Klöckner aliwasili mjini Kiev kwa usafiri wa treni na ziara yake haikutangazwa kutokana na sababu za kiusalama. Alipokewa na mwenyekiti wa bunge la nchi hiyo Ruslan Stefanchuk, na hapo baadaye atakutana na rais Volodymyr Zelensky.
Klöckner pia alitembelea kituo cha nishati ya umeme, ili kuona athari iliyosababishwa na mashambulizi ya Urusi nchini humo yaliyolenga miundombinu ya nishati na kuwaacha wakaazi wengi katika baridi kali kipindi hiki cha majira ya baridi.