1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Turathi za Syria zipo hatarini kupotea

8 Julai 2013

Kutekwa miji mikubwa na kuharibiwa sehemu za makumbusho nchini Syria, ni tishio kwa turathi za kitamaduni za nchi hiyo wakati huu wa vita kati ya waasi na vikosi vya utawala wa Assad

Turathi za Syria
Turathi za SyriaPicha: picture-alliance/dpa

Mkurugenzi mkuu wa shirika la umoja wa mataifa kuhusu elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Irina Bokova amekosoa uharibifu unaoendelea katika mji wa zamani wa Aleppo, sehemu ambao ulitangazwa kuwa ni turathi ya Ulimwengu tokea mwaka 1986, miongoni mwa sita nchini Syria.

Usemi wa zamani unaosema''kalamu ina nguvu kulikoni upanga, bado unaonekana kuwa na ukweli na hii ni kutokana na kila wiki waandamanaji katika mji mdogo wa Syria Kafranbel wakichora mabango na kuandika vipeperushi kupinga utawala wa Rais wa Syria Bashar al-Assad

Hata hivyo maelfu ya mabango hayo na vipeperushi yametumwa Marekani kupitia juhudi za wanaharakati za kuhakikisha ushahidi huo unahifadhiwa kwa ajili ya kizazi kijacho.

Daktari Shadi Latta aliyeko mji wa Illinois Marekani ambaye amezaliwa na kukulia mji wa Kafranbel amesema amepokea mara ya kwanza mabango 100 mwezi Februari mwaka huu, mara ya pili alipokea seti kadhaa za mabango na anatarajia kupokea zaidi ya mia moja hivi punde tu.

Shadi Latta amesema mabango hayo na vipeperushi yanaondoshwa Syria na kuhifadhiwa nchini Uturuki kablaya kuyasafirisha kwa meli kwenda Marekani akiongeza kuwa kuyatoa mabango ndani ya nchi ndiyo njia pekee ya kuyahifadhi.

Raed Fares mwenye umri wa miaka 41 mtetezi wa fikra hiyo amesema kwa waliopo mjini Kafranbel, mabango hayo na vipeperushi vimekuwa sehemu muhimu ya historia ya Syria kwa ajili ya kizazi kijacho na hivyo kuna haja ya kuhifadhiwa.

"Katika wakati wa kuwapo mashambuzi na mabomu huwezi kujua ni lini unaweza kupoteza vyote," amesema Fares ambaye anaishi mjini Kafranbel akiongeza kutokana na hali hiyo walifikiria bora kusafirisha mabango hayo kwenda Marekani kwa usalama na hiyo ni njia pekee ya kuwzesha wao kuzifikia jamii za kimataifa na kufikisha ujumbe wao huko.

Lengo likiwa ni kuonesha mabango hayo mwshoni mwa mwezi Julai mjini New York. Hivyo uoneshaji wa mabango hayo umefanikiwa kupatikana kiasi ya Dola 650,000 ambazo zinatumwa Syria kupitia misaada ya kibinadamu.

Utumaji wsa mabango na vipeperushi hivyo Marekani kwa sasa si kazi rahisi, hata hivyo kazi hiyo ilianza wakati Fares, ambaye alikuwa anasomea utabibu katika chuo kikuu cha Aleppo alipojiunga na Ahmad Jalal, msanii ambaye alikubali kutengeneza mabango hayo kuanzia mwaka 2011.

Fares anasema licha ya utawala wa Asaad kufuatilia kwa kakaribu watu wanaompinga Assad na waandamanaji kwa kuchoma moto mabango hayo baada ya maandamano, lakini wakagundua kuwa kuchora mabango hayo ni sehemu ya historia ya matukio nchini Syria na hivyo kuna haja ya kuyahifadhi badala ya kuyaharibu.

Wakati mji wa Kafranbel ambao una watu wanaokadiriwa kufikia chini ya watu 20,000, ulipoingia mikononi mwa waasi, Fares na Jalal waliamua kufungua ofisi yao mjini humo.

Kituo hicho kinachoitwa "kituo cha habari-" kwa sasa ni ofisi yao ya kazi , chenye jenereta la umeme na kompyuta za mkononi na kugeuka pia kituo cha waandishi wa habari wa kigeni wanaofika mjini Kafranbel.

Umoja wa mataifa tayari umekadiria vifo nchini tokea lilipoanza vuguvugu la upinzani dhidi ya Rais assad,mwezi Machi mwaka 2011 kufikia karibu watu 93,000. Lakini bado Latta na Fares wana matumaini kuwa hatimae ushindi utakuwa wao na kwamba mwisho wa Rais Assad unakaribia.

Mwandishi: Hashimu Gulana/IPS

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman