Turk: Vita mjini El- Fasher ni doa kwa jamii ya kimataifa
14 Novemba 2025
Matangazo
Akifungua kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu El-Fasher, Kamishna Mkuu wa Haki za Binaadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema jamii ya kimataifa haijaingilia kati licha ya ripoti za mara kwa mara za "ukatili wa kutisha" na kuwaonya wahusika kuwa watawajibishwa.
Turk ameonya kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imeashiria kuwa inafuatilia hali hiyo kwa karibu.
''Wote waliohusika katika mzozo huu wanapaswa kujua. Tunawatazama na haki lazima itendeke. Sudan imejikuta katika vita vya uwakilishi wa raslimali asili na mali zake. Nchi nyingi katika eneo hilo na kwingineko zinahusika.''
Rasimu ya azimio inayojadiliwa leo Ijumaa inalaani aina zote za uingiliaji kutoka nje unaochochea mzozo huo.