1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Polisi Uturuki imewakamata watu 110 kwa tuhuma za ugaidi

25 Aprili 2023

Polisi nchini Uturuki imewakamata leo watu 110 wanaohusishwa na makundi ya wapiganaji.

Türkei Ankara Polizeieinsatz
Picha: Tunahan Turhan/Zuma/IMAGO

Duru za usalama pamoja na za chama kinachowaunga mkono Wakurdi zinasema wanasiasa, wanasheria na waandishi wa habari ni miongoni mwa waliokamatwa katika misako hiyo ambayo imehusishwa na uchaguzi wa Mei 14. Operesheni hiyo iliangazia mji wa Diyarbakir, ambao ndio mji mkubwa wa eneo la kusini mashariki mwa Uturuki lenye wakaazi wengi wa Kikurdi, na kuwalenga watu katika mikoa 21 walio na mafungamano na kundi la wanamgambo lililopigwa marufuku la Chama cha Wafanyakazi wa Kikurdi - PKK. Msako huo umefanyika ikiwa ni chini ya wiki tatu kabla ya uchaguzi wa urais na ubunge ambao ni mtihani mkubwa kabisa kwa Rais Recep Tayyip Erdogan tangu alipoingia madarakani mwaka wa 2002.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW