Tusk aanza uwaziri mkuu wa Poland kwa mara nyengine
13 Desemba 2023Matangazo
Bunge lilipiga kura ya kuwa na imani na serikali ya Tusk siku ya Jumanne (Disemba 12), ambapo kwenye hotuba yake ya ufunguzi, kiongozi huyo alitowa wito wa mshikamano baina ya pande hasimu za kisiasa nchini humo.
Tusk, anayefuata siasa za mrengo wa kati, aliwahi kuwa waziri mkuu wa Poland kutoka mwaka 2007 hadi 2014, alipochaguliwa kuwa rais wa Baraza la Ulaya, nafasi aliyoishikilia hadi mwaka 2019.
Soma zaidi: Wabunge wa Poland wanajiandaa kuipigia kura serikali ya Tusk
Sasa amerudi madarakani akiongoza muungano wa vyama vya siasa vilivyoshinda uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, kwa ahadi za kuirejesha Poland kwenye majukwaa ya kimataifa.