1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tusk: Nitapambana kuisadia Ukraine dhidi ya Urusi

12 Desemba 2023

Waziri Mkuu mteule wa Polanda Donald Tusk, amesema anapanga kuishawishi Magharibi kutoa usaidizi zaidi kwa Ukraine kuisaidia kupambana na uvamizi wa Urusi.

Waziri Mkuu mteule wa Polanda Donald Tusk
Waziri Mkuu mteule wa Polanda Donald TuskPicha: Czarek Sokolowski/AP/dpa/picture alliance

Katika taarifa yake bungeni wakati alipoliwasilisha baraza lake la mawaziri, amesema hatowasikiliza wanasiasa wa Magharibi waliochoshwa na suala la Ukraine.

"Nataka kusema kwamba ni jukumu la Poland, jukumu la serikali mpya,  na pia ni jukumu letu sote kusema kwa sauti na uwazi kabisa kwamba jumuiya yote ya Mataifa ya Magharibi inaonyesha kujitolea kuisaidia Ukraine katika vita hivi. hicho ndicho nitakachokifanya kuanzia siku yangu ya kwanza kama Waziri Mkuu" Alisema Tusk

Soma pia:Tusk aahidi kuendelea kuisaidia Ukraine

Poland imekuwa muungaji mkono mkubwa kijeshi na kisiasa wa Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi Februari mwaka jana. Tusk ambaye ni rais wa zamani wa Baraza la Ulaya aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Poland jana Jumatatu. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW