1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Tusk atetea mpango wa kusitisha haki ya kuomba hifadhi

15 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk ametetea mpango wa kusitisha haki ya kuomba hifadhi nchini humo huku mashirika ya haki za binadamu na asasi za kiraia zikisema kuwa haki za kimsingi lazima ziheshimiwe.

Waziri mkuu wa Poland Donald Tusk akihudhuria mkutano wa waandishi wa habari baada ya mkutano na waziri mkuu wa Latvia Evika Silina mjini Warsaw mnamo Februari 29, 2024
Waziri mkuu wa Poland Donald TuskPicha: Kuba Atys/Agencja Wyborcza.pl via REUTERS

Katika ujumbe alioandika katika mtandao wa kijamii wa X, Tusk amesema ni haki na jukumu lao kulinda mpaka wa Poland pamoja na ule waUlaya na kuongeza kuwa usalama wake hautajadiliwa.

Tusk alitangaza mpango huo wake wa kusitisha haki ya wahamiaji kuomba hifadhi wakati wa kongamano la Muungano wake wa Kiraia siku ya Jumamosi. Hiyo ni sehemu ya mpango utakaowasilishwa kwenye kikao cha baraza la mawaziri hii leo Jumanne.

Soma pia;Poland yapanga kusitisha kwa muda haki ya kuomba hifadhi

Hata hivyo uamuzi huo hautawaathiri raia wa Ukraine ambao wamepewa ulinzi wa kimataifa nchini Poland.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa takriban watu milioni 1 kutoka Ukraine wamekimbia vita nchini humo kuingia Poland.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW