1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tutaijibu Marekani kwa nyuklia - Pyongyang

4 Machi 2023

Korea Kaskazini imesema itakabaliana na kile inachokiita "uchokozi wa Marekani" na washirika wake kwa kutumia silaha zake za nyuklia ikidai ndilo jibu sahihi kwa uchokozi huo.

Nordkorea Machthaber Kim Jong mit seiner Tochter im Stadium in Pjöngjang
Picha: KCNA/REUTERS

Korea Kaskazini imeilaumu Marekani kwa kile ilichosema ni "kusambaratika kwa mifumo ya kimataifa ya udhibiti wa silaha" na kusisitiza kuwa silaha za nyuklia za Pyongyang ni jibu stahiki ili kuhakikisha amani na utulivu katika rasi ya Korea.

Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kaskazini imesema kupitia shirika la habari la serikali, KCNA, kwamba Marekani, Korea Kusini na Japan wamekuwa wakivuka mstari mwekundu na kwamba hali hii kamwe haiwezi kuvumiliwa.

Soma zaidi: Marekani na Korea Kusini zatafakari kutanua Luteka za Kijeshi
Kim Jong Un aombwa kuzungumza na mrithi wake Suk Yeol

Hayo ni baada ya Marekani na Korea Kusini kutangaza hapo jana kuwa zitafanya luteka ya pamoja ya kijeshi ya siku 10, kuanzia Machi 13. 

Mazoezi hayo ya kijeshi yamekuwa yakiibua hisia kali kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo imekua ikitoa vitisho vya kutumia silaha za nyuklia.  

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW