Tuzo la Nobel la Amani
11 Desemba 2010Mwanaharakati raia wa China ambaye yuko kifungoni Liu Xiabo ametunukiwa tuzo ya amani ya Nobel katika sherehe ambazo hakuhudhuria na badala yake palikuwa na kiti kitupu na picha yake.
Akiwa gerezani anakotumikia kifungo cha miaka 11, Liu alisema tuzo hiyo iwaendee waliofariki mnamo mwaka 1989 katika uwanja wa Tiananmen.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya Nobel,Thorbjorn Jagland ametoa wito wa kuachiliwa Liu haraka.
Serikali ya China haikumruhusu yeyote aliye na uhusiano na Liu kwenda Oslo na imelitaja tuzo hiyo kuwa udanganyifu wa kisiasa. China inaonekana kuzuwia mitandao ya habari ya nchi za magharibi, na vyombo vya habari vya taifa havikuzitaja sherehe hizo isipokuwa kutoa taarifa ya kushutumu tuzo hiyo.
Kilele cha sherehe hizo kilikuwa ni maandamano ya kuwasha mwenge mjini Oslo.
Mwandishi:Maryam Abdalla/Rtre
Mhariri:Sekione Kitojo.