1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu wa 2011 watatunukiwa wakinamama watatu shupavu

7 Oktoba 2011

Tume ya Nobel imetaka kutoa jaza kwa juhudi za wakinamama za kupigania amani, na demokrasia bila ya matumizi ya nguvu barani Afrika na arabuni

Washindi wa tuzo ya amani ya Nobel kutoka kulia:rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia,Tawakkul Karman wa Yemen na Leymah Gbowee wa LiberiaPicha: dapd/DW-Montage

Wanawake watatu wametunukiwa mwaka huu tuzo ya amani ya Nobel kutokana na" juhudi zao za kupigania bila ya mtutu wa bunduki, usalama wa akina mama na haki yao ya kuchangia kikamilifu katika kuleta amani". Rais Ellen Johnson-Sirleaf wa Liberia, mkuu wa shirika lisilomilikiwa na serikali la "Mtandao wa akina mama kwa ajili ya amani na Usalama barani Afrika" - Leymah Gbowee, na mwanaharakati wa haki za wakinamama nchini Yemen Tawakkul Karman. Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 2004 kwa tuzo ya amani ya Nobel kutunukiwa wakinamama barani Afrika. Wanawake 15 wameshatunukiwa tuzo hiyo ya amani hadi wakati huu. Uamuzi wa ajabu wenye kutoa risala ya nguvu.

Watabiri wa mambo na safari hii pia wamekosea:Tuzo ya amani ya Nobel hajatunukiwa si kansela wa zamani wa Ujerumani Helmut Kohl na wala si Umoja wa ulaya. Watatunukiwa wakinamama watatu mashujaa wa kutoka Afrika na Yemen. Kwa namna hiyo tume ya waamuzi ya Nobel imetoa ishara bayana: katika kuimarisha demokrasia na amani, wakinamama wanastahiki kubeba jukumu la maana. Tangu barani Afrika mopaka katika ulimwengu wa kiarabu.

Rais Ellen Johnson Sirleaf wa LiberiaPicha: dapd

Uamuzi wa tume ya Nobel unaonyesha wazi kabisa hakuna tena sababu kwa wanawake baada ya maandamano na vuguvugu la kupigania uhuru kukimbilia tena katika familia zao na katika mazingira yao ya kawaida, kama hali inavyodhihirika kuwa katika nchi za kiarabu. Wanawake wote watatu wamebainisha: Pekee kuwajibika kwa muda mrefu kisiasa na kijamii, ndio chanzo cha kutambuliwa na kuhifadhiwa masilahi na haki ya wakinamama katika jamii.

Liberia ni mfano mwema kuweza kuigizwa katika nchi nyingi za dunia. Kama inavyodhihirika katika vita vingi kote ulimwenguni, wanawake ndio wanaobeba mzigo mzito zaidi wa vita vya miaka 14 vya wenyewe kwa wenyewe. Matokeo ya kutisha: watu laki mbili na nusu wamepoteza maisha yao, milioni moja wameyapa kisogo maskani yao na wahanga wasiojulikana idadi wa matumizi ya nguvu na ubakaji.

Ellen Johnson Sirleaf ameingia madarakani mwaka 2006 akikabidhiwa mojawapo ya majukumu magumu kabisa ya kisiasa kuwahi kushuhudiwa ulimwenguni.

Bila ya kuwa na uoga na kwa ukakamavu, amepambana na rushwa na mitindo ya kujipendelea, ameanza kuwanyanyua na kuwaongoza katika maisha ya kawaida wananchi walioathirika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo. Hakutishika kwa vishindo vya wale wanaojinata kuwa wababe wa kisiasa wala rushwa. Ameitakasa nchi yake kwa namna ambayo mara kadhaa amekuwa akipokea risala za kutaka kumuuwa.

Tuzo ya mwaka huu kwa wanawake watatu ni ushahidi pia wa wajibu wa kisiasa na kijamii katika kupigania amani na uhuru. Mbali na mwanasiasa Johnson Sirleaf, kuna wanawake wengine wawili wakakamavu wanaotokana na mashirika ya huduma za jamii. Bibi mwenye umri wa miaka 40, Leymah Roberta Gbowee, ambaye ni mkuu wa shirika lisilomilikiwa na serikali la "Mtandao wa akina mama kwa ajili amani na Usalama barani Afrika na mwanaharakati kijana anayepigania haki za akina mama katika jamii ya kihafidhina ya Yemen, Tawakkul Karman. Wafuasi wa itikadi kali ya dini ya kiislam wanamtuhumu kutaka kuwachochea wanawake wafanye uasi dhidi ya wanaume. Mwenyekiti huyo wa jumuiya ya "Waandishi habari wa kike wasiokuwa na minyonyoro" daima amekuwa akipigania "kuheshimiwa haki za kimsingi, akipinga matumizi ya nguvu na ndoa za kulazimishwa na kupigania haki ya kuwakilishwa wakinamama katika harakati za kisiasa. Hayo hayo amekuwa akiyapigania pia mwanaharakati wa haki za binaadam wa Liberia, Gbowee.

Mwanaharakati wa haki za wakinamama nchini Yemen Tawakkul KarmanPicha: dapd

Tuzo ya amani ya Nobel inatudhihirishia jambo muhimu kabisa nalo ni kwamba bila ya kuheshimiwa haki za wakinamama na kujumuishwa kwao kikamilifu katika juhudi za kuleta amani na demokrasia amani, hakuna kokote kule duniani ambako amani na demokrasia vitaweza kuendelea milele.

Mwandishi:Ute Schaeffer(DW Afrika)/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Josephat Charo

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW