Tuzo ya Mo-Ibrahim
19 Oktoba 2009Matangazo
Taasisi ya Mo Ibrahim imeshindwa kumpata mshindi wa tuzo ambayo huwatunza viongozi bora wa Afrika waliomaliza muda wao madarakani kwa kutoa mfano juu ya demokrasia na utawala bora, imeshindwa kumpata mshindi wa tuzo hiyo ya dola milioni 5 kwa mwaka huu wa 2009. Mmoja kati ya wajumbe wa jopo la waamuzi ni Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Dr Salim Ahmed Salim. Mohamed AbdulRahman alizungumza naye kwa simu kutoka London na kwanza alimuuliza sababu za taasisi hiyo kushindwa kumpata mshindi mwaka huu .
Mtayarishaji: Mohammed Abdulrahman
Mhariri: Josephat Charo