Tuzo ya Ujerumani na Afrika yaenda Tanzania na Madagascar
28 Novemba 2018Kwa nini mara hii lakini tuzo hiyo imetolewa kwa wanaharakati wa ulinzi wa mazingira. Mkuu wa jopo la majaji kwa ajili ya tuzo hiyo Volker Faigle ameweka wazi wakati wa hotuba yake, kwamba mwanamfalme wa Uingereza wiki chache zilizopita alipokuwa akifungua mkutano wa kimataifa alitoa wito wa kuzuwia matumizi ya kupindukia ya ardhi ili kuzuwia athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Ni wito muhimu kama anavyoeleza rais wa majaji Volker Faigle waliowachagua wanaharakati hao wawili wa kulinda mazingira kutoka Afrika.
"Jioni ya leo sisi ni mashahidi , wa watu hawa ambao wameweza kujitolea na kupambana na hali hii kutoka katika bara ambalo ni jirani yetu la Afrika. Watu ambao wanataka kuwalinda watoto wao pamoja na watoto wetu na nchi zao. Pamoja na kuilinda sayari yetu na kuonesha hatari inayokabili uasili pamoja na wanyamapori. Na wanajihusisha pamoja na kupambana ili kupata sheria ya ulinzi kwa hayo yote."
Kuanzia mwaka 1993 wakfu wa Ujerumani na Afrika umejionesha kuwa unapigania amani , demokrasia na maendeleo endelevu. Rais wa bunge la Ujerumani Wolfgang Schaueble ameeleza kuhusu umuhimu wa bara la Afrika kwa Ulaya. Amesema hali ya baadaye ya bara la Ulaya itaamuliwa kupitia ushirikiano wa pamoja wa maendeleo zaidi ya bara la Afrika.
Hali bora ya Afrika
Afrika inahitaji haraka hali bora ya kiuchumi , lakini haiwezi kufanya hivyo peke yake. "Hii inahusika zaidi na usalama wa muda mrefu wa msingi wa maisha ya watu katika bara hilo. Mapambano kuhusu ulinzi wa uhai anuai pamoja na wanyama na mimea ni muhimu , na ulinzi katika mabadiliko ya tabia nchi ni jukumu muhimu kwa dunia nzima."
Schaeuble amesema pia kwamba wanaharakati hao ambao wamepata tuzo hii , Gerald Bigurube na Clovis Razafimalala wanahatarisha mambo mengi binafsi.
"Wanahatarisha mambo mengi ya binafsi. Biashara haramu inayoingiza fedha nyingi ya miti ya liwa nchini Madagascar , pamoja miradi mikubwa ambayo inataka kuharibu maeneo ya wanyama na mimea nchini Tanzania."
Bigurube mwenye umri wa miaka 66 amekuwa tangu miaka 40 iliyopita ni mwanaharakati wa ulinzi wa mazingira nchini Tanzania, ambaye amehusika zaidi katika eneo maarufu duniani la mbuga ya Serengeti. Kwanza alikuwa mkuu wa shirika la taifa la hifadhi ya wanyamapori la TANAPA, na hivi sasa ni mkurugenzi wa jamii ya maeneo ya zoo mjini Frankfurt.
Jaji wa tuzo hiyo Faigle anamsifu kuwa ni mjenga muhimu wa daraja. Bigurube anasimama kwa ajili ya ulinzi endelevu wa mazingira, ambayo yanakwenda kwa pamoja na mahitaji muhimu ya jamii na maendeleo.
Mwandishi: Daniel Pelz /ZR/ Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Khelef