1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UAE yakana kubainika idadi kubwa ya silaha Sudan

14 Agosti 2023

Umoja wa Falme za Kiarabu umekanusha ripoti zinazodai kwamba zimegundulika silaha katika shehena ya mizigo ya msaada wa nchi hiyo kwa wakimbizi wa vita vya Sudan.

Bürgerkrieg im Sudan | Grenzstadt Gallabat zu Äthiopien
Picha: AFP

Umoja wa falme za kiarabu umesema haugemei upande wowote katika mgogoro wa Sudan. Waangalizi wamesema pande zote mbili zilizoko vitani nchini Sudan,jeshi la serikali likiongozwa na AbdelFattah el Burhani na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdani Daglo anayeongoza kikosi cha wanamgambo cha RSF wanaongozwa na mataifa  ya kigeni huku Misri ikiwa upande wa Burhani na Umoja wa Falme za kiarabu ukiegemea kambi ya Daglo.Hata hivyo jana Jumapili mkurugenzi wa mawasiliano katika wizara ya mambo ya nje ya UAE  Afra Al Hameli amesema nchi yake haijawahi kupeleka silaha kwa upande wowote katika vita vya Sudan tangu ulipozuka mgogoro huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW