UAE yakemea mashambulizi ya Israel yaliyofanywa Qatar
12 Septemba 2025
Matangazo
Umoja huo pamoja na Bahrain ndio nchi za mwanzo kabisa kurejesha mahusiano yao na Israel mwaka 2020 na wamekuwa wakikosoa hatua ya taifa hilo katika vita vyake na Hamas mjini Gaza.
"Reem bint Ebrahim Al Hashimy, Waziri wa ushirikiano wa Kimataifa wa UAE alimuita Naibu Balozi wa Israel David Ohad Horsandi, kukemea mashambulizi ya Qatar na kauli za uhasama zinazotolewa na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Al Hashimy alimkumbusha Horsandi, kuwa uchokozi wowote unaofanywa kwa nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la nchi za Ghuba GCC linachukuliwa kama shambulizi kwa mataifa yote wanachama.
Hata hivyo ujumbe wa Israel huko haujatoa maoni yoyote juu ya hilo.