Pistorius kubakia gerezani
20 Agosti 2015Matangazo
Haijafahamika ikiwa bodi hiyo itaweza kukutana tena, kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya sheria Mthunzi Mhaga, lakini hakuna uwezekano kuwa uamuzi mpya utafikiwa kabla ya Ijumaa ambayo ndiyo tarehe ya awali aliyostahili kuachiliwa.
Pistorius, ambaye ni mwanariadha wa Olimpiki anayetumia miguu ya kubandika, anatumikia hukumu ya kifungo cha miaka mitano kwa kumuua bila kukusudia mchumbake Reeva Steenkamp mwka wa 2013. Angeweza kuhamishwa kutoka jela na kupewa kifungo cha nyumbani baada ya kutumikia kipindi cha miezi kumi jela, ambacho kinakamilika Ijumaa.
Wkaati ikipinga hatua hiyo ya kuachiliwa Pistorius, wizara ya sheria imesema uamuzi huo umetolewa mapema.
Mwandishi: Bruce Amani/APE
Mhariri: Iddi Sessanga