1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UASI MPYA MAGHARIBI MWA SUDAN

23 Desemba 2003
KHARTOUM: Rais Omar el-Bashir wa Sudan ameliomba bunge lirefushe kile kipindi cha hali ya hatari kwa mwaka mmoja mwingine.Ametoa ombi hilo licha ya kwamba matumainio yanazidi kuongezeka kuwa hivi karibuni kutapatikana makubaliano ya kuvimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka ishirini nchini Sudan.El-Bashir amesema ingawa kuna matumainio ya kupatikana amani pamoja na SPLA-waasi wa eneo la kusini,lakini sasa serikali inakabiliwa na uasi mpya katika eneo la magharibi la Darfur.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW