China yawataka raia wake kuondoka mpakani mwa Myanmar
28 Desemba 2023Wito huo umetokana na kile Beijing ilichokitaja kuwa hatari ya usalama wakati makundi ya uasi wa makabila ya wachache yakipambana na utawala wa kijeshi.
Waasi hao wameteka miji kadhaa na vituo muhimu vya mpakani venye umuhimu wa kibiashara na China, katika kile ambacho wachambuzi wanasema ndiyo changamoto kubwa zaidi ya kijeshi kwa utawala wa kijeshi tangu uliponyakua madaraka mwaka 2021.
Mapema mwezi huu Beijing ilisema iliratibu mazungumzo ya upatanishi kati ya jeshi na makundi matatu ya uasi na kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano kwa muda.
Hata hivyo makabiliano yameendelea katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Shan, huku kundi mojawapo la waasi la Jeshi la Ukombozi la Ta'ang, TNLA, likidadi kuteka miji mwili zaidi katika siku za karibuni.