Ubelgiji yakumbuka miaka 10 ya shambulio la kigaidi
22 Machi 2026
Wafanyakazi na timu ya waokoaji walikusanyika katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Brussels wakishikana mikono wakiunda laini ndefu kabla ya bao la ukumbusho kufunguliwa na mfalme Philippe na waziri Mkuu wa Ubelgiji Bart De Wever.
Muda mfupi baadae misa ya kuwakumbuka walioaga dunia ikafanyika katika kituo cha treni za chini za Maelbeek.
Mashambulizi hayo yanadaiwa kufanywa na watu watatu wakujitolea muhanga kutoka kundi la dola la kiislamu IS, waliojiripua katika uwanja huo wa ndege na katika kituo hicho cha treni.
Watu 36 waliuwawa na wengine 340 walijeruhiwa. Katika kumbukizi hiyo Waziri Mkuu De Wever aliishukuru timu ya kutoa huduma za dharura kwa kuwasaidia watu haraka na kuwahimiza kutokata tamaa.
Amesema siku zote Ugaidi unatumika kuwagawa watu na kuwatia hofu, lakini miaka 10 baadae kinachoonekana ni mshikamano, ubinaadamu na utu.