1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Albania-Wapiga kura wasubiri matokeo

4 Julai 2005

Tirana:

Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Albania baada ya uchaguzi wa bunge hapo jana. Wachunguzi wanasema uchaguzi huo umefanyika katika hali ya utulivu, huko Rais Alfred Moisiu akiwaambia wananchi wake kwamba ulikua ni uchaguzi huru na wa haki kuwahi kuonekana katika historia ya Albania, akiwa na matumaini kwamba hali hiyo imefungua njia katika takwa lake la kujiunga na Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya kujihami ya magharibi-NATO. Tume kuu ya uchaguzi imekionya chama tawala cha Kisoshalisti na kile cha upinzani cha Democratic dhidi ya matamshi ya kujitangazia ushindi kabla ya matokeo rasmi. Matokeo ya awali yanatazamiwa kutangazwa baadae leo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW