Uchaguzi Australia
21 Agosti 2010Vituo vya kupigia kura vimefungwa katika maeneo yenye watu wengi, huko Australia, huku matokeo ya awali yakionyesha kuwa Waziri Mkuu Julia Gillard anayeongoza chama cha Leba, huenda akapata ushindi dhidi ya mpinzani wake Tony Abbot anayeongoza muungano wa wahafidhina. Kulingana na matokeo hayo ya kituo cha televisheni cha kitaifa, Leba ina asilia mia 51 ya kura ukilinganisha na asilia mia 48 ya muungano huo wa Kiliberali. Kulingana na wachambuzi wa chama cha Leba, Gillard huenda akashinda kwa wingi wa viti vinne katika bunge lenye viti 150 nchini Australia. Huku vyama vyote viwili vikionekana kuwa na sera sawa za mambo ya nje, haiba ya wagombea inasemekana itakuwa suala nyeti la kuwavutia asilia mia 10 ya wapiga kura wapatao milioni 14, Australia.