1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Belarus: Lukashenko akabiliwa na changamoto kali

8 Agosti 2020

Baada ya miaka 26 madarakani, kiongozi Muimla wa Belarus Alexander Lukashenko anakabiliwa na changamoto kubwa zaidi ya utawala wake wakait akiwania muhula wa sita. Hali ngumu ya uchumi na janga la Covid vyampa mtihani.

Weißrussland | Belarus | Präsident Alexander Lukaschenko hält eine Rede
Picha: imago images/Russian Look/V. Lisitsyn

Hali ya kutoridhika kuhusian na uchumi unaozidi kudorora na uitikiaji wa serikali kuhusu janga la virusi vya corona vimesaidia kuchochea mikutano mikubwa kabisaa ya upinzani nchini humo tangu Alexander Lukashenko alipokuwa rais wa kwanza na wa pekee kuchaguliwa kufuatia kuporomoka kwa Muungano wa Kisovieti.

Tetesi miongoni mwa tabaka la watawala na mzozo mkali na Urusi, ambayo ndiyo mfadhili na mshirika mkubwa zaidi wa Belarus, vimeongeza ugumu katika kampeni ya kuchaguliwa tena kwa mkurugenzi huyo wa zamani wa kampuni ya serikali mwenye umri wa miaka 65, siku ya Jumapili.

Lukashenko, ambaye aliwahi kupewa jina la utani la "Dikteta wa mwisho barani Ulaya" katika mataifa ya magharibi kutokana na ukandamizaji wake dhidi ya upinazni, ameweka wazi kwamba hatosita tena, ikihitijaka, kutumia nguvu kusambaratisha jaribio la wapinzani wake kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais.

Soma zaidi: Lukashenko ashinda urais kwa mara ya tano, Belarus

Maafisa wa tume ya uchaguzi waliwazuwia wapinzani wakuu wawili wa rias kutoka kile ambacho hivi sasa kimekuwa mchuana wa watu watano. Sviatlanta Tsikhanouskaya, mwalimu wa zamani wa mwenye umri wa miaka 37 na mke wa mwanablogu wa upinzani alieko gerezani, amefanikiwa kupata uungwaji mkono imara, akivutia mamia kwa maelf kwenye mikutano yake ya kampeni.

Svetlanta Tikhanovsakaya, mgombea wa upinzani anaempa changamoto rais Alexander Lukashenko.Picha: Imago Images/ITAR-TASS/N. Fedosenko

'Ishara ya mabadiliko'

Katika mahojiano na shirika la hahari la Marekani la Associated Press, Tsikhanouskaya alijielezea kama "ishara ya mabadiliko" "ilikuwa inatokota kwa ndani kwa zaidi ya miaka 20," alisema Tsikhanouskaya.

"Tuna hofu kila wakati na hakuna anaethubutu kusema neno. Hivi sasa watu wanachagua ishara ya mabadiliko."

Tsikhanouskaya amezunguka nchi, akitumia ukatishwaji tamaa wa umma na uitikiaji wa Lukashenko juu ya janga la virusi vya corona, na kudorora kwa uchumi wa taifa hilo unaofanana na enzi za kisoviet.

Rais huyo ameupuuza ugonjwa wa virusi vya corona na kuutaja kuwa "uwendawizimu" na amekataa kunazisha hatua za kuzuwia kusambaa kwa ugonjwa huo, akisema Wabelarus wanaweza kujilinda dhidi ya ugonjwa huo kwa kutumia kileo cha vodka, kutembelea sauna na kufanya kazi kwa bidii mashambani.

Soma pia: Rais Lukashenko ashinda uchaguzi nchini Belarashia

"Walikuwa wanatuambia kwamba virusi hivyo havipo na kuvipuuza kama uwendawazimu huku maelfu ya Wabelarus wakiugua," alisema Diana Golubovich, 54, wakili aliehudhuria mkutano wa Tsikhasnouskaya mjini Brest, mji ulioko kwenye mpaka wa nchi hiyo na Polanda.

"Ghafla kila moja alitambua kwamba taifa la kisoshalisti ambalo Lukashenko alikuwa akijivunia halipo."

Belarusi, taifa la wakaazi milioni 9.5, limeripoti zaidi ya visa 68,000 vilivyothibitishwa na vifo 580 katika janga la covid-19. Wakosoaji wameituhumu serikali kwa kudanganya kuhusu tarakimu ili kushusha idadi ya vifo.

Lukashenko alitangaza mwezi uliopita kwamba alikuwa ameambukizwa na virusi hivyo lakini hakuwa na dalili za covid-19 na alipoma haraka, akidai ni kutokana na kufanya michezo. Alitetea ushughulikiaji wake wa mlipuko huo, akisema hatua ya kufungwa kwa shughuli ingeharibu uchumi dhaifu wa taifa hilo.

Rais Lukashenko akitoa hotuba yake ya kila mwaha kuhusu hali ya taifa mjini Minsk, Agosti 4, 2020.Picha: Getty Images/AFP/Belta/A. Pokumeiko

Mdororo wa kiuchumi Belarus

Belarus bado imepata pigo kubwa baada ya mteja wake mkuu wa mauzo ya nje Urusi, kuingia katika mdororo uliosababishwa na janga la corona, na masoko mengine ya kigeni kushuka. Kabla ya janga la virusi vya corona, uchumi wa taifa hilo unaodhibitiw ana serikali ulikuwa tayari umekwama kwa miakakadhaa, na hivyo kuchochea hasira za umma.

"Lukashenko hana mpango wa kuiendeleza nchi. Ameondoa uhuru wa kisiasa, na sasa anawanyima watu fursa ya ukuaji wa kiuchumi," alisema Valery Tsepkalo, balozi wa zamani wa Belarus nchini Marekani, aliekuwa amepnga kupambana dhidi ya Lukasheko kwenye uchaguzi lakini akakimbilia nchini Urusi pamoja na watoto mwezi uliyopita kuepuka kukamatwa. "Hiyo ndiyo sababu kuu ya maandamano."

Baada ya kuanza kwa kampeni za urais, serikali iliendesha ukandamizaji dhidi ya wapinzani kwa ari mpya. Zaidi ya washiriki 1,300 wa maandamano wamekamatwa tangu Mei, kwa mujibu kituo cha haki za binadamu cha Viasna. Mkuu wa kampeni wa moja ya wagomea alikamatwa nje ya kituo cha kupigia kura siku ya Ijumaa na kuhukumiwa kifungo cha siku 10 jela kwa madai ya kuandaa mkutano mkubwa usiyoruhusiwa.

Soma pia Lukashenko aonya dhidi ya maandamano ya uchaguzi

Waangalizi wa kisiasa wanasema kampeni ya uchaguzi pia imeonyesha migawiko miongoni mwa tabaka la wasomi wa Belarus huku baadhi yao wakijiunga na siasa kwa mara ya kwanza.

Pamoja na balozi wa zamani Tsepkalo, mkuu wa benki kubwa inayodhibitwa na Urusi alifikira kugombea dhidi ya Lukashenko. Mpinzani huo maarufu, Viktor Babariko, alifungwa mwezi Mei kuhusiana na madai ya utakatishaji fedha na ukwepajikodi, madai aliyopinga na kusema yalichochewa kisiasa.

Lukashenko na mshirika wake wa karibu, Rais Vladmir Putin wa Urusi.Picha: picture-alliance/AP Photo/T. Zenkovich

Katika kile ambacho upinzani wa kisiasa na wadadi wengi huru wanakichukulia kama jaribio la kuimarisha uungaji mkono wa umma kwa rais wa sasa unaoporomoka, maafisa wa Belarus waliwakamata wakandarasi 33 wa kijeshi kutoka Urusi na kuwashtaki kwa mipango ya kupanga "maandamano ya watu wengi."

Kukamatwa kwa Warusi hao kuliashiria uongezeko lisilokifani katika mzozo kati ya Belarus na Urusi, ambazo mara nyingi zinakuwa na mizozo ya mara kwa mara licha ya uhusiano wao wa karibu.

Soma pia Belarus yavutana na mshirika wake wa jadi Urusi

Wakati Urusi na Belarus ziliposaini makubaliano ya muungano mwaka 1996, Lukashenko alitaka kuyatumia kama njia ya hatimaye kuongoza taifa lililoungana kama mrithi wa rais aliekuwa anaugua, Boris Yelstin. Lakini mabo yalibadilika baada ya Vladmir Putin kuwa rais mwaka 2000; kiongozi huyo wa Belarus alinza kukataa kile alichokionakama shinikizo la Kremlin kuchukua udhibiti wa Belarus.

Urusi haitaki kumuondoa Lukashenko bali kumdhoofisha

Alexander Klaskovsky,  mchambuzi huru mwenye makao yake mjini Minsk, alisema anafikiri Kremlin inatumai kampeni zenye mihemko nchini Belarus zitasaidia kuondoa udhibiti wa Lukashenko kwenye madaraka na kumfanya akubali wazo la muungano wa mataifa hayo mawili.

Urusi na Belarus zaanza Luteka kubwa ya Kijeshi

02:15

This browser does not support the video element.

"Moscow haina haja ya kuondolewa kwa Lukashenko, lakini inataka kumdhoofisha kwa kiwango kikubwa ili atoke katika kampeni hizo uhalali wake ukiwa umedhoofika, uhusiano ulioharibika na mataifa ya magharibi na uchumi ukiwa katika hali mbaya," alisema Klaskovsky. Lukashenko aliedhoofika atakuwa zawadi kwa Moscow."

Wakati maafisa wa uchaguzi wana uwezekano mkubwa wa kumtangaza Lukashenko kuwa mshindi kwa kishindo, matatizo yake hayataishia kwenye uchaguzi.

"Itakuwa karibu asilimia 80 ya kura kwa Lukashenko, ili watu wake wasifikiri kuwa kiongozi amekuwa dhaifu," alitabiri. Serikali ina rasilimali za kutosha na nvugu ya kukatili kubakisha madaraka na kukandamiza maandamano, lakini inakosa majibu ya swali kuu kuhusu njia ya Belarus kufikia maendeleo. Lukashenko atashinda bila shaka, lakini utakuwa ushindi wa mizengwe."

Chanzo: APE

Mhariri: Zainab Aziz

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW