1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Georgia:

28 Machi 2004

TIFLIS:
Kwa mara ya kwanza tangu uangushwe utawala wa Rais Eduard Shevardnadse wapiga kura nchini Georgia hii leo wanachagua bunge jipya. Inatazamiwa kuwa chama cha Rais Mikhail Saakashvili kitanyakua ushindi mkubwa katika uchaguzi huo wa bunge mjini Tiflis. Waangalizi wanafikiri hakuna chama chochote kingine kitakachoweza kuvuka mpaka wa asili miya saba ya kura kuviwezesha kuingia bungeni. Pia yanangojewa matokeo ya uchaguzi katika mkoa wa Absharia unaowania kujitenga na serikali kuu ya Tiflis. Uchaguzi huu ni marudio ya uchaguzi uliofanyika majira ya mapukutiko mwaka jana ambayo matokeo yake yalibishwa na upinzani uliomshutumu Rais Shevardnadse kufanya kiini macho cha kura. Shevardnadse alijiuzulu baada ya kufanyika maandamano makubwa ya upinzani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW