1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi mdogo Zanzibar unaakisi ushindani wa kisiasa?

27 Oktoba 2023

Ushindani wa kisiasa umeibuka tena kufuatia uchaguzi mdogo, jimbo la Mtambwe kisiwani Pemba iliko ngome ya aliekuwa mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Maalim Seif Sharif Hamad.

Mpiga kura akitumbukiza karatasi kwenye sanduku la kura
Mpiga kura akitumbukiza karatasi kwenye sanduku la kuraPicha: Emmanuel Herman/REUTERS

Vyama vinne vinashiriki katika uchaguzi huo mdogo wa kumtafuta mwakilishi wa jimbo hilo baada ya kufariki aliyekuwa mwakilishi wake, Habib Mohammed Ali, mapema mwaku huu, lakini mchuano wa wazi ni baina ya chama CCM na washindani wao na washirika wenzao kwenye serikali ya Umoja wa Kitaifa,  ACT Wazalendo.

Kampeni zilitawaliwa na mtizamo wa hali za maisha ambapo wakati CCM kinaomba kuungwa mkono na wapiga kura kutokana kile inachodai "kuendelea kuleta maendeleo."

Huku chama cha ACT kikisema CCM haifai kupigiwa kura kwa sababu imeshindwa kuzuia kupanda kwa gharama za maisha.

Soma pia:Uendeshaji bandari ya Zanzibar rasmi mikononi mwa muwekezaji

Akifunga kampeni za chama chake cha ACT Wazalendo, makamu mwenyekiti wa chama hicho na makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, aliwataka wapigakura kukipa ushindi chama hicho:

Kwa upande wake, Chama cha Mapinduzi, CCM, kupitia makamo wa pili wa rais, Hemed Suleiman Abdulla, kimeomba wapiga kura kuunga mkono chama hicho ili kumpa nguvu zaidi Rais Mwinyi kuwatumikia.

Chaguzi ndogo kipimo cha demokrasia?

Uchaguzi huu mdogo wa Mtwambwe unafanyika baada ya chaguzi nyengine mbili ndogo kisiwani Pemba, iliko ngome ya muda mrefu ya upinzani.

Mpiga akiwekea alama ya wino baada ya kupiga kuraPicha: Emmanuel Herman/REUTERS

Wa kwanza ulikuwa wa jimbo la Pandani ambapo Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC, iliitangaza ACT kwa ushindi kwa kura chache zaidi kuliko inavyokuwa kwenye chaguzi za kisiwani humo.

Mwengine ulikuwauchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Konde, ambao ulilazimika kurejewa tena baada ya awali, Tume ya Uchaguzi, ZEC, kumtangaza mgombea wa CCM kuwa mshindi. 

Soma pia:Wahamiaji wapewa uraia visiwani Zanzibar

Uchaguzi wa kesho pia una umuhimu mkubwa kwa Rais Hussein Mwinyi kuona ni kwa kiasi gani anaungwa mkono katika jitihada zake za kuleta maendeleo.

Na vile vile ni kipimo kwa viongozi wapya wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ambayo sasa ina wajumbe wawili kutoka ACT Wazalendo, chini ya uwenyekiti wa Jaji George Kazi, ambaye ametowa wito kwawapiga kura kuzingatia sheria na kuweka mbele suala la amani.

Jumla ya wapiga kura 6,098 wanatarajiwa kupiga kura zao hapo kesho na matarajio ya kutangazwa kabla ya kumalizika mapumziko ya mwisho wa wiki.
 

Mbowe azungumzia katiba na tume ya uchaguzi

01:00

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW