Zuma atarajia kuwa rais .
22 Aprili 2009JOHANNESBURG.
Watu wa Afrika Kusini leo wanapiga kura katika uchaguzi mkuu ambapo chama kinachotawala ANC kinatarajiwa kushinda na hivyo kumpitisha rais wa chama hicho Jacob Zuma kuwa kiongozi wa nchi vilevile.Bwana Zuma amesema chama cha ANC kinatarajia idadi kubwa ya wapiga kura katika uchaguzi huo.
Akizungumzia juu ya chama kipya cha upinzani Congress of the People, Zuma ameeleza kuwa chama hicho kimekipa nguvu mpya chama chake cha ANC.
Zuma amesema chini ya uongozi wa ANC katika miaka 15 iliyopita chama hicho asilani hakijatumia wingi wake bungeni kubadili katiba ya nchi na hakina mpango wa kufanya hivyo katika siku za usoni. Chama cha ANC kinadhibti theluthi mbili ya viti bungeni.
Hatahivyo kura za maoni zinaonesha kuwa chama hicho kitapoteza baadhi ya viti katika uchaguzi wa safari hii.
Wananchi milioni 23 wa Afrika Kusini wamejiandikisha kupiga kura.