1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Uchaguzi Mkuu unaosubiriwa Venezuela kufanyika mwezi Juni

6 Machi 2024

Maafisa wa Venezuela wametangaza kuwa uchaguzi mkuu unaosubiriwa kwa shauku nchini humo utafanyika mnamo Juni 28 mwaka huu.

Venezuela | Nicolas Maduro
Rais Nicolas Maduro wa Venezuela anatazamiwa kuwania muhula mwingine madarakani wakati wa uchaguzi wa mwezi Juni. Picha: Ariana Cubillo/AP Photo/picture alliance

Tangazo la tarehe hiyo ya uchaguzi limetolewa na rais wa tume ya taifa ya uchaguzi Elvis Amoroso. Uamuzi huo wa kufanya uchaguzi mwezi Juni umekwenda sambamba na matakwa ya upinzani ulioshinikiza kuwepo muda wa kutosha kuboresha daftari la wapigakura na vyama kujitayarisha kwa kampeni.

Rais Nicolas Maduro anatazamiwa kuwania muhula mwingine madarakani. Hata hivyo mpinzani wake mkuu Maria Corina Machado bado amepigwa marufuku kushiriki uchaguzi huo.

Mnamo mwezi Januari Mahakama ya Juu ya Venezuela ilipilia msumari uamuzi wa kumzuia Machado kushiriki uchaguzi kwa miaka 15 baada ya kutiwa hatiani kwa kushiriki njama ya kula rushwa.