UCHAGUZI MPYA BAADA YA SIKU 45
25 Novemba 2003TBILISI: Siku moja baada ya Eduard Shevardnadze kujiuzulu kama rais wa Georgia,upande wa upinzani ulioshika madaraka umetangaza kuwa kutafanywa uchaguzi mpya wa rais na bunge katika kipindi cha siku 45 zijazo.Kwa wakati huo huo rais wa mpito Nino Burdzanadze ametoa muito kwa viongozi kuanza kuchukua hatua za kurejesha hali ya kawaida nchini baada ya kuwepo maandamano ya upinzani kwa majuma kadhaa.Kuambatana na ripoti za wanadiplomasia,Russia na Marekani zimepiga simu mara kadhaa kuhakikisha kuwa hatua ya kubadilishwa serikali inatekelezwa kwa usalama nchini Georgia.Wachambuzi wa kisiasa wanasema Russia inataka kuhakikisha kuwa hakutokuwepo machafuko mapya katika mpaka wake wa kusini.Na Marekani nayo ikidowea mafuta na gesi kutoka Azerbaijan,inataka kuhakikisha kuwa bomba la kusafirishia mali hiyo litapitia Georgia likielekea Bahari ya Kati.
