1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi nchini Kongo waingia siku ya pili

21 Desemba 2023

Wapiga kura nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaingia siku ya pili ya uchaguzi mkuu ambao umekumbwa na matatizo makubwa ya utekelezaji wa zoezi hilo na kusababisha baadhi ya vituo vya kupigia kura kutofunguliwa.

Uchaguzi wa Kongo
Raia wa Congo wakipiga kura mjini Kinshasa Picha: Alain Uyakani/Xinhua/IMAGO

Wapiga kura wanamchagua rais, wabunge na wajumbe wa serikali za mitaa. Rais aliyemo madarakani Felix Tshisekedi, anagombea muhula wa pili.

Upigaji kura ulicheleweshwa kwa kiwango kikubwa hapo jana, nchini kote.

Tume ya uchaguzi bado inajaribu kupeleka vifaa kwenye vituo vya kupigia kura vilivyopaswa kufunguliwa muda mrefu.

Kwa nini uchaguzi ni muhimu DR Kongo?

Mkuu wa tume ya uchaguzi (CENI) Denis Kadima, amesema kwenye televisheni ya taifa kwamba watu watapiga kura leo Alhamisi kwenye maeneo ambayo hayakuweza kupiga kura hapo jana.

Watu milioni 44 wamejiandikisha kupiga kura katika nchi hiyo yenye jumla ya watu milioni 100.  Matokeo ya uchaguzi yatatangazwa baada ya siku kadhaa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW