Uchaguzi nchini Msumbiji
31 Oktoba 2009Matangazo
MAPUTO:
Nchini Msumbiji, Rais Armando Guebuza na chama chake cha Frelimo wanaongoza katika chaguzi za rais na bunge. Baada ya kuhesabiwa nusu ya kura zilizopigwa,Guebuza amejikingia asilimia 78 ya kura hizo na chama chake asilimia 77.
Chama cha Frelimo kilitazamiwa kushinda tangu hapo awali kwa sababu upande wa upinzani una mivutano. Hata Guebuza ametarajiwa kuchaguliwa tena. Hii itakuwa awamu yake ya pili madarakani. Chama cha Frelimo kinatawala tangu Msumbiji ilipopata uhuru wake kutoka Ureno katika mwaka 1975.
Matokeo ya mwisho ya uchaguzi yanatazamiwa kutangazwa rasmi tarehe 12 Novemba.