Uchaguzi Nigeria wakaribia.
19 Machi 2007Kwa mara ya kwanza taifa hilo la Afrika magharibi lililondamwa na historia ya mapinduzi ya kijeshi, litashuhudia rais aliyechaguliwa akimkabidhi madaraka mrithi wake atakayechaguliwa pia kwa njia ya kidemokrasi.
Yote yanatarajiwa kwenda salama salimini: kwamba kutakuweko na mabadiliko ya kirafiki na kidemokrasia ya utawala nchini Nigeria ,lakini kuna wanaotaka kuona demorasia katika nchi hiyo baadae mwaka huu inapata pigo.
Haya ishara zake zinaonekana katika masuala mengi. Barani Afrika Nigeria ni nchi yenye utajiri mkubwa miongoni mwa zinazotoa mafuta. Ikiwa na jumla ya wakaazi 130 milioni, mabadiliko ya utawala kwa njia ya kidemokrasi yatachangia katika utulivu wa eneo hilo zima. Ni wazi kuwa bado kuna wanaotawala kiimla, kama Robert Mugabe wa Zimbabwe, Laurent Gbagbo wa Ivory Coast au Paul Biya wa Cameroun.
Lakini Afrika sasa ina balozi. Uungaji mkono kwa Rais Olusegun Obasanjo ni muhimu. Rais wa Ujerumani Horst Kohler au mjumbe wa Kansela wa zamani Schröder aliyehusika na masuala ya Afrika Uschi Eid, walikua sahihi walipomtaja kuwa nguzo ya mwanzo mpya barani Afrika. Ni sawa kabisa lakini pia ni wajibu wa Wanigeria wenyewe kuona hilo linafanyika.
Wiki nne kabla ya uchaguzi huo, maandalizi yamo katika vurugu. Kote nchini pande zinazohusika zinaendesha kampeni ya hadi umwagaji damu. Haya yasingewezekana kama tume ya uchaguzi isingekua chombo cha rais aliye madarakani. Kutokana na hayo tayari wanigeria wengi wanahisi , matokeo yameshapangwa na chama cha Obasanjo-Peoples Democratic.
Miezi kadhaa sasa chama hicho kimekua katika jitihada za kuhujumu uchaguzi safi na awa haki. Miongoni mwa mbinu zinazotumiwa ni kujaribu kuwanunua wabunge. Obasanjo amefanikiwa pia kuhakikisha mtu aliyemtaka Umaru Yar Ádua anakua mgombea. Makamu wa rais Abubakar Atiku amejiunga na upinzani akisimama kuwa mgombea urais.
Hayo hayakumpendeaza Obasanjo na kumezuka hali ya kushutumiana kuhusu visa vya rushwa. Tume ya uchaguzi imeingia katika kindumbwe ndubwe hicho na kumkatalia Atiku ruhusa ya kuwa mgombea kwa shutuma hizo za rushwa. Matokeo haya yanakumbusha miaka ya nyuma pale tume ya uchaguzi nchini Ivory coast ilipomkatalia ruhusa mgombea wa upinzani kuwania uchaguzi.
Nigeria imo katika hatari ya kuingia katika vurugu: Na kuna mawili, ama mahakama iupe haki upinzani na tume kuuahirisha uchaguzi, Au tume inaweza kuipuuza mahakama na kuendelea na uchaguzi kwa msaada wa idara ya usalama inayodhibitiwa na Obasanjo.
Chama tawala cha Obasanjo kina nafasi nzuri ya kushinda uchaguzi kuliko cha mgombea wa tatu mwenye nguvu na mtawala wa zamani wa kijeshi Muhamamad Buhari, kwa kuwa kina mtandao wa kisiasa kote nchini, lakini ikiwa kitaweka mazingira safi. La sivyo matokeo yatkua ni pigo kwa demokrasia nchini Nigeria na Afrika kwa jumla.
Ndiyo maana serikali ya Ujerumani na pia umoja wa ulaya hawapaswi kukaa kimya. Ni muhimu kuinusuru demokrasaia isiporomoke nchini Nigeria.