1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPoland

Uchaguzi Poland: Morawiecki na Tusk wadai kushinda

16 Oktoba 2023

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki, amedai kuwa´chama chake tawala cha kizalendo Sheria na Haki (PiS), kimeshinda uchaguzi wa ubunge uliofanyika Jumapili.

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki
Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki Picha: Maciek Jazwiecki/Agencja Wyborcza.pl via REUTERS

Hata hivyo, Morawiecki hakubainisha kwamba anafikiri chama chake kitaweza kuunda serikali.

Kiongozi wa PiS Jaroslaw Kaczynski, amewaambia wafuasi wao kwamba japo kupata asilimia 37 ya kura ni mafanikio makubwa, huenda isitoshe kushika madaraka.

Kiongozi wa muungano wa upinzani Donald Tusk, naye amedai kuwa vyama vitatu vya upinzani vimepata kura za kutosha kushinda uchaguzi mkuu.

Vyama hivyo vya upinzani viliwania kwa tiketi tofauti lakini kwa ahadi zilizofanana, za kuondoa chama tawala cha Sheria na Haki mamlakani na kurejesha uhusiano mzuri na Umoja wa Ulaya.

Haijabainika wazi ikiwa vyama hivyo vitatu vya upinzani (Civic Coalition, Third Way na the New Left ) viko tayari kuungana kuunda serikali.