Uchaguzi Tanzania: Wagombea wapiga kura
28 Oktoba 2020mwendo wa saa moja asubuhi vituo vingi vya kupigia kura vilifunguliwa ili kutoa nafasi kwa raia waliokidhi vigezo kwa mujibu wa katiba ya taifa hilo lla Afrika mashariki, kutekeleza zoezi la kuchagua viongozi ambao ni madiwani, wabunge na rais watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Rais john magufuli ambae anatetea kiti chake kwa muhula wa pili na wa mwisho baada ya kupiga kura yake wilayani chamwino mkoani Dodoma amesifu hali ya utulivu ambayo imekuwepo katika zoezi hili la uchaguzi na kusisitiza juu ya haja ya kutunza amani ya nchi wakati na baada ya kukamilika kwa mchakato huo wa kidemocrasia.
Wakati rais magufuli akikamilisha zoezi hilo, mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya chama kikuu cha upinzani chadema Tundu lisu alitarajiwa kupiga kura katika jimbo lake la nyumbani la singinda mashariki mkoani Singida katikatika mwa Tanzania.
Zoezi la kunakili namba ya mpiga kura katika daftari la kupigia kura haliridhishi
Mgombea wa chama cha wananchi cuf Profesa Ibrahim Lipumba ambae amepiga kura yake jimbo la kawe jijini Dar es salaam ameelezea kutoridhishwa na utaratibu wa kunakili namba ya mpiga kura katika karatasi ya kupigia kura.
kwa upande wake mgombea wa chama cha ADC Queen Sendiga baada ya kupiga kura yake ameonesha kufurahishwa na utaratibu wa kujumuisha makundi ya watu wenye ulemavu katika uchaguzi huu hasa wasioona, kwa kuwekea karatasi maalum za nukta nundu.
katika hatua nyingine ya kustajabisha mgombea urais wa chama cha UPDP Twalib Kadege ameshindwa kupiga kura katika kituo cha sisimba jijini Mbeya baada ya kufika hapo akiwa hana kitambulisho cha mpiga kura.
Japo kuwa zoezi hili linalowashirikisha watu milioni 29 wenye vigezo limeanza kwa amani na utulivu, kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya mawakala wa vyama vya upinzani kuzuiliwa kuingia katika vituo vya kupiga kura wakitajwa kutokidhi vigezo. zoezi la kupiga kura linatarajiwa kukamilika majira ya saa kumi jioni na matokeo yanataajiwa kuanzaa kutangazwa muda mfupi baada ya hapo.
Mwandishi: Hawa Bihoga Dar Es Salaam