Uchaguzi Tanzania
31 Oktoba 2010Watanzania wanapiga kura hii leo katika uchaguzi wa urais ambao huenda ukampa uongozi kwa mara ya pili na ya mwisho , rais aliyepo madarakani Jakaya Kikwete katika nchi hiyo iliyo ya pili kwa ukubwa kiuchumi,Afrika mashariki.
Rais Kikwete alichaguliwa kwa wingi wa asilimia 80.2 ya kura mnamo mwaka 2005 na wakati maoni ya awali ya wapiga kura yalimpa nafasi kubwa ya uongozi , hali hiyo imepadilika katika wiki za mwisho za kampeni na baadhi ya wachambuzi wanadai kuwa idadi kubwa ya wananchi wanaoatarajiwa kujitokeza kupiga kura huenda wakapiga kura zao kwa upinzani.Tanzania ni nchi iliyo imara katika eneo ambalo kwa mara nyengine hukosa utulivu na imefanikiwa kufanya chaguzi za vyama vingi vya kisiasa mara tatu tangu mwaka 1995, baada ya utawala wa zaidi ya miongo mitatu wa chama kimoja.
Mpinzani mkuu wa rais Kikwete katika uchaguzi huu, Wilbrod Slaa wa chama cha CHADEMA, ametoa wito kwa wapiga kura kumpa nafasi ya kupambana na rushwa na kuendeleza huduma kama vile za afya na elimu katika nchi hiyo iliyo maskini.
Mwandishi Maryam Abdalla/RTRE.
Mhariri:Sekione Kitojo.