Uchaguzi Tanzania
6 Novemba 2010Matangazo
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameapishwa rasmi hii leo kuiongoza nchi hiyo katika kipindi cha pili cha miaka mitano, baada ya kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo.
Tume ya Uchaguzi ya Taifa-NEC ilitangaza matokeo hapo jana ambapo ilisema Rais Kikwete ameshinda kwa kupata asilimia 61 ya kura, katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.
Hata hivyo, kiongozi wa upinzani kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Dr. Wilbrod Slaa anataka kura zihesabiwe tena kwa madai kuwa kulifanyika udanganyifu. Chama tawala cha Rais Kikwete cha CCM, kimekuwa madarakani tangu Tanzania ilipopata uhuru wake mwaka 1961.
Mwandishi Maryam Abdalla/dpae,rtre
Mhariri:Dahman Mohammed